Kocha wa Klabu ya Uingereza ya Arsenal, Unai Emery ameeleza kujutia namna ambavyo alimtilia shaka Mohammed Salah kujiunga na timu hiyo alipokuwa akikipiga Paris Saint-Germain (PSG).

Emery ameeleza kuwa walikuwa na mpango wa kumsajili Salah lakini walikuwa na shaka kidogo, ndipo mchezaji huyo alipotua Liverpool Juni 2017 na baadaye kuishangaza dunia kwa uwezo wake.

Kocha huyo ambaye leo klabu yake itakung’utana na Liverpool inayoongoza Ligi, ameeleza kuwa endapo wangemsajili Salah leo wangekuwa wamemsajili mmoja kati ya wachezaji bora zaidi duniani.

“Tulizungumza kuhusu uwezekano wa kumsajili Salah kutoka PSG alipokuwa anacheza Roma. Lakini tulikuwa na shaka kwenye baadhi ya mambo na baadaye akaenda Liverpool. Sasa hivi hayo mashaka hayapo tena,” alisema Emery.

“Kwa sasa kama utawataja wachezaji bora watano duniani, Salah ni mmoja wao. Kama tungemsajili leo, tungekuwa tumemsajili mchezaji aliye kwenye nafasi tano za juu duniani,” aliongeza.

Salah amejipatia mafanikio makubwa Uingereza, na mwaka huu alitajwa katika nafasi ya sita ya tuzo ya Mchezaji Bora wa Soka duniani (Ballon d’Or). Tuzo hiyo ilienda kwa Luka Modric aliyemaliza ufalme wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi .

Jaji Mutungi kuteta na viongozi wa siasa nchini
Video: JPM awajaza noti wastaafu, Makonda aibua dude Dar