Msanii wa Muziki wa kizazi kipya kutoka jijini Mwanza, Edu boy amefungua studio yake mpya jijini humo kwa lengo la kuwasaidia wasanii wachanga ambao bado hawajatambulika katoka katika Tasnia ya Muziki.

Akizungumza na Clouds Fm katika kipindi cha XXL Edu boy amefunguka kuwa ameamua kufungua studio yake mwenyewe jijini humo ambayo iko maeneo ya Kirumba ili aweze kwasaidia wasanii hao.

‘’Nimeamua kufungua studio ya kwangu mwenyewe ambayo ipo maeneo ya Kirumba jijini Mwanza na nimeona nitoe fursa kwa wasanii wote ambao hawajatoka kurekodi bure’’amesema Edu boy.

Aidha, ameongeza kuwa sababu hasa ambazo zimepelekea kufungua Studio hiyo ni kutimiza ahadi yake ya kuwainua wasanii wa nyumbani ili kuonyesha uzalendo zaidi hasa kwa wazawa wa jiji hilo ambako ndiko anakotoka.

Hata hivyo, amesema kuwa ametoa fursa hiyo kutokana na ugumu na changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakizipitia wasanii wachanga hasa pale  wanapokuwa wanatafuta njia ya kutokea katika muziki.

Video: Sitaomba radhi kamwe kuhusu kilichotokea Clouds Media-Makonda
Video: Ruge azungumza haya baada ya kukutana na Makonda, Jukwaa la Wahariri