Mchekeshaji Ebitoke ameeleza chanzo cha kuvamia na kufanya fujo juzi kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliokuwa umeandaliwa na muigizaji mwenzake, Yusuph Mlela aliyekuwa mpenzi wake.

Ebitoke amefanya mahojiano maalum na Dar24 ambapo ameeleza kuwa kilichomsukuma ni hasira zilizotokana na kutopewa vitu anavyomdai, alivyompa walipokuwa wapenzi.

”Nilikubali, ukikubali hauwezi ukapata shida, mi nilishakubali kuachana nae,” Ebitoke aliiambia Dar24.

“Lakini kuna kitu anakijua nataka ndio maaana nafanya hizi fujo, wala hata sina shida naye, fujo zangu zote kuna kitu nataka aniletee, tuwe sawa tuwe na waashikaji kabisa,” aliongeza.

Mchekeshaji huyo pia amedai kuwa endapo hatatimiziwa hilo na msanii huyo, atamchafua kwakuwa anazijua siri zake zote.

Ebitoke alivamia mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Mlela na kumshambulia mwanamke anayedaiwa kuwa ni mpenzi mpya wa msanii huyo.

Angalia mahojiano yote hapa:

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Novemba 13, 2019
Nugaz: Shabiki wa yanga asiyenunua jezi orijino, anahujumu timu, ''Ndio maana hatulipi madeni''

Comments

comments