DSTV inayowajali wateja wake imeamua kuja na ofa kabambe mwezi huu wa Januari inayoenda kwa jina la “KITU JUU YA KITU”.

Ambapo ofa hii ya kitu juu ya kitu ni ofa itakayomnufaisha mteja moja kwa moja bila kuongeza gharama yeyote ambapo kila mteja atakayelipia kifurushi chake atapandishwa daraja kwenda kifurushi cha juu yake ndani ya muda wa masaa 48.

Akieleza Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja wa Multichoice Tanzania, Hilda Nakajumo amesema kuwa endapo mteja atalipia kifurushi cha Bomba cha 19,000 atapewa chaneli ambazo ni za kifurushi cha Family cha  thamani ya 29,000, vivyo hivyo kwa ambae atalipia kifurushi cha Family cha 29,000 atapewa za kifurushi cha Compact cha thamani ya 44,000.

Katika uzinduzi huo kabambe wa msanii mkongwe wa bongo fleva, Dully Sykes amekula shavu kushirikiana na DSTV katika kuitangaza ofa hiyo ambapo alipopata nafasi ya kuzungumza Dully amesema anajivunia kufanya kazi na DSTV na atakuwa bega kwa bega kuitangaza ofa hiyo kwa watanzania ili wajue namna gani DSTV inawajali wateja wao na kwenda nao sambamba.

Aidha, Mkuu wa kitengo cha masoko wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo  amesema ofa hiyo ni ya aina yake hivyo ameomba watanzania kutumia nafasi hiyo kwani ni kwa ajili yao, pia wataendelea kupata burudani mbalimbali pamoja na kutazama ligi mbalimbali kwa bei nafuu kabisa.

”Mteja atakayelipia 29,000 atapandishwa hadi kifurushi cha 44,000 hivyo ataweza kushuhudia ligi kubwa duniani ikiwemo michezo yote ya ligi kuu Uingereza bila kusahau Laliga, Serie A na michuano mingine mikubwa ulimwenguni” amesema Shelukindo.

Ofa hiyo itadumu mpaka mwisho wa mwezi februari.

Tanga yang'ara miradi kwa njia ya 'Force Account'
Rais wa Congo atishia kuvunja Bunge

Comments

comments