Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linasema, limewauwa waasi zaidi ya 80 wa ADF Wilayani Beni, katika operesheni dhidi ya makundi ya waasi.

Operesheni hii inayokuja, baada ya waasi hao kuendelea kutekeleza mauaji ya raia zaidi ya 100 tangu mwezi Novemba, katika Wilaya hiyo na kuzua wasiwasi kuhusu usalama wa wakazi wa Beni.

Katika wiki za hivi karibuni, Beni ilikumbwa na matukio mablimbali hasa, mauaji ya raia, ambapo kundi la waasi wa Uganda la ADF lilishtumiwa kuhusika na mauaji hayo ya kikatili.

Ufilipino: Hofu yazidi kutanda Kimbunga Kammuri

Wananchi Mashariki mwa nchi hiyo wameendelea kuandamana kulaani ukosefu wa usalama, wakishinikiza kuondoka kwa jeshi la Umoja wa Mataifa MONUSCO kwa madai kuwa, limeshindwa kuwalinda.

Hivi karibuni Rais Felix Tshisekedi Tshilombo aliapa kuyatokomeza makundi yanayohatarisha usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiwa ni pamoja na kundi hilo la waasi wa Uganda la ADF.

Tanzania, Namibia zajidhatiti kukuza sekta ya biashara
Ufilipino: Hofu yazidi kutanda Kimbunga Kammuri

Comments

comments