Drake ameweka wazi kuwa amewahi kupanga kuachana na muziki akiwa kileleni kutokana na alichowahi kuona kwa wasanii wengine.

Akifunguka katika mahojiano ambayo yalimhusisha LeBron James kwenye kipindi cha ‘The Shop’ cha HBO, Drake alisema kuwa moja kati ya vitu anavyojali zaidi kwenye muziki wake ni jinsi ya kuachana nao.

“Nadhani kitu kikubwa ninachokifikiria kwenye muziki wangu ni namna ya kuachana nao kwa amani na heshima,” alisema Drake.

“Nimekuwa naona kuna watu wanakaa muda mrefu zaidi ya wanavyostahili, na staki kuwa mtu wa namna hiyo. Hii inatokana na kubaki na mawazo ya ushindi, kuwa na fikra za watu kubaki na kitu ambacho bado wanakipenda na kufikia hatua ambayo ninawalisha kitu na wanakubali,” alisema.

Ni kama Drake anataka kustaafu kwa heshima, akiwa kileleni na anapendwa.

Albam zake za mwisho, ‘Thank Me Later’, ‘Take Care’, ‘Views’ na ‘Scorpion’ zote zimefanya vizuri.

LeBron James pia alimuunga mkono Drake, akieleza kuwa ni vyema mtu kufikia hatua ya kuacha kile unachokifanya kabla mshale haujaanza kushuka chini.

“Unapaswa kuwa na mtu ambaye anakwambia, ‘aisee unapaswa kukubaliana na kidogo utakachokipata sasa au kuachana na hii kitu wakati huu,” alisema.

Drake bado ana mengi hata nje ya muziki, hivi karibuni ameendelea kuwekeza katika vipindi vya televisheni kama ‘Top Boy’ na series za HBO ya ‘Euphoria’.

Kanye west asifu kofia ya Rais Trump
Viongozi wa vyama vya ushirika watiwa mbaroni