Janjaro ambaye awali alikuwa anaitwa Dogo Janja alikuwa na kila sababu ya kufurahi zaidi jana kwenye kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa baada ya kukabithiwa zawadi ya gari.

Janja-3

Rapa huyo amepewa zawadi hiyo na uongozi wa Tip Top Connection ambao umekuwa ukimlea kimuziki hadi jana alipofikisha umri wa miaka 21.

Ameshare picha za zawadi hiyo kwenye mitandao ya kijamii na kuonesha jinsi alivyofurahishwa na zawadi hiyo.

Gari

“Shukran Sana Mshua @madeeali Uko Mbalii Lakini Umenisuprise.. Sina Cha Kukulipa Zaidi Ya Kukuheshimu Daima.. Hakika saiv Barabarani Tutapigiana Honiii Tu Shukran Sanaaa Sanaa Sanaa MUNGU AKUWEKE,” aliandika Janjaro.

TFF Yafanya Mabadiliko Kwenye Kamati Ndogo
Godbless Lema Amgeukia Wema Sepetu