Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbord Slaa amekemea tabia ya baadhi ya Watanzania kubeza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano huku akibainisha kuwa vitendo vya kutumia mitandao ya kijamii kukosoa utendaji wa serikali unawapa shida mabalozi kuitetea nchi huko walipo,kwasababu vitendo hivyo vinawakatisha tamaa wahisani wanaotaka kuisaidia Tanzania.

Ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Startv wakati wa ziara ya mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali duniani walipokuwa wakitembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR eneo la Soga Mkoani Pwani.

Ametoa mfano kutokana na kauli aliyoitoa kiongozi flani ambaye hakumtaja imesababisha watalii 100 kutoka Sweden kuahirisha safari ya kuja Tanzania kwa ajili ya kutalii.

Hata hivyo, Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali wapo katika ziara ya kutembelea na kujionea miradi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano kwa fedha za ndani.

LIVE DAR ES SALAAM: Rais Magufuli akihutubisha katika mkutano wa wakuu wa nchi za SADC
RC apiga marufuku watumishi kwenda likizo