Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajia kuongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kinacho tarajiwa kufanyika Septemba 18 mwaka huu kujadili hali ya kisiasa Zanzibar.

Katika Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Waride Bakari Jabu, imesema kuwa kikao hicho cha siku kwaajiri ya kupokea na kujadili kwa kina taarifa ya hali ya kisiasa ya Zanzibar pamoja na taarifa nyingine mbali mbali kutoka Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.

Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa kikao hicho kitapokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika ngazi za Wilaya kwa kipindi cha 2017-2022, kwa upande wa Zanzibar na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa

Hata hivyo, Imeelezwa kuwa kikao hicho kimetanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC – Zanzibar kilichofanyika Septemba 16, mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdulla Juma Saadalla “Mabodi”

Mambosasa: Tunaendelea kuwakamata wanaomuombea Lissu
Van Nistelrooy amtabiria makubwa Lukaku

Comments

comments