Mbunge wa Jimbo la Busega kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Raphael Chegeni ametoa msaada wa Vyerehani, Mashine za kufyatulia matofali na kusaga nafaka zenye thamani ya zaidi ya milioni 32.5.

Ametoa msaada huo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli za kuliletea maendeleo taifa.

Amesema kuwa ametoa msaada huo ili kuweza kuwasaidia wananchi waweze kujikwamua na wimbi la umasikini na kusaidia nchi kufikia malengo ya kuwa na uchumi kati ambao utawawezesha wananchi kukuza uchumi wao.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Busega, Tano Mwera amemshukuru mbunge huyo kwa kuwawezesha wanawake na vijana kwani kupitia vifaa hivyo wanaweza kujikwamua kiuchumi na kuunga mkono falsafa ya rais Dkt. Magufuli.

Hata hivyo, katika sherehe hiyo ya siku ya wanawake duniani, vikundi za ishirini na tano vimenufaika kwa kila kikundi kupata shilingi laki tano kwaajili ya kuendeleza mitaji na shughuli zao mbalimbali wanazozifanya.

 

Polisi wamtwanga mashtaka 16 muigizaji wa ‘Empire’
Kupungua kwa bei ya bidhaa kwanusuru mfumuko wa bei.

Comments

comments