Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro na timu yake kufanya uchunguzi wa kina juu ya mauaji yaliyotokea Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Ametoa agizo hilo Mkoani Kagera Wilaya ya Muleba wakati wa uzinduzi wa uandikishaji wa vitambulisho vya taifa mkoani humo.

Aidha, Dkt. Nchemba amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kujua undani wake ili kuondoa hofu iliyotanda kwa wananchi kulingana na matukio yanayoendelea kutokea.

“Mataifa mengine mtu akiuawa shughuli zote zinasimama, tusiweke haya mazoea ya watu wanapotea potea kama mtu kapuliza dawa ya mbu, hili si jambo la kawaida, wafanye uchunguzi kwa kina kujua nani amehusika na tukio hilo,”amesema Nchemba

Hata hivyo, ameongeza kuwa masuala ya Demokrasia huamliwa kwa kalamu na si mapanga, malungu wala mikuki, hivyo ni lazima uchunguzi ufanyike kubaini wahusika wote.

Kamanda Mambosasa atoa tahadhari kuhusu uchaguzi
Chadema yakanusha kususia uchaguzi