Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Njombe kupitia chama cha mapinduzi CCM Dkt. Susan Kolimba, amewahamasisha Wanawake wa UWT mkoani humo kuunda vikundi vya kitarafa ili waweze kufanya Shughuli za pamoja za kuboresha uchumi.

Ameyasema hayo Wilayani Makete aliposhiriki kikao cha Baraza la Umoja wa Wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Wilayani humo na kutumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wanawake hao kuunda vikundi vya Kitarafa.

Amesema kuwa lengo la kuhamasisha uundaji wa vikundi hivyo ni kuwawezesha wanawake hao mkoani Njombe, kujikwamua kiuchumi ikiwa pamoja na kujenga uwezo wa kujitegemea katika kuendesha shughuli zao kiuchumi.

Aidha, wilaya ya Makete inajumla ya Tarafa sita, ambapo Dkt. Kolimba ameanza kwa kuziwezesha Tarafa Tatu jumla ya Tsh, 1,500,000/= huku akiahidi kuziwezesha tarafa tatu zilizobaki na Wilaya ya Ludewa inajumla ya Tarafa tano ambazo ameziwezesha Tarafa zote Jumla ya Tsh, 2,500,000/= katika Vikundi vya Wanawake.

Vikundi hivyo vya Kitarafa vimepata kiasi cha Tsh, 500,000/= kila kimoja ikiwa ni hatua za awali za kuwahamasisha na kuwaunga mkono Wanawake hao katika kuibua vyanzo vya kiuchumi na kuviendeleza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo Wilaya ya Makete, Erica Sanga amesema kuwa mchango wa Dkt. Kolimba kwa Wanawake hao ni mkubwa ambao utawawezesha kusisimama wenyewe kiuchumi na kuendesha shughuli zao.

Nao wajumbe walioshiriki Kikao hicho kutoka Kata zote za Wilaya ya Makete, wamemshukuru Dkt. Kolimba kwa kutambua umuhimu wa Wanawake katika Jamii, na kuamua kuwasaidia fedha kwaajili ya kuibua Miradi itakayo wasaidia kuendesha familia zao.

Jeshi la Sudan ‘lakubali yaishe’, wananchi washerehekea
Lampard alamba dili Chelsea