Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa anawajua viongozi wanne ambao ni vigogo walioshiriki katika kupanga mauaji ya mhamasishaji wa utalii nchini Wayne Lotter.

Ameyasema hayo hii leo mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu wizara hiyo na masuala ya utalii.

Dkt. Kigwangalla amevitaka vyombo vya usalama kuhakikisha vinawakamata vigogo hao mapema iwezekanavyo na kuwa kama hawatafanya hivyo basi yeye atafikisha taarifa kwa Rais John Pombe Magufuli.

Amesema katika kipindi cha siku 100, Wizara yake imebaini mitandao 74 ya watu wanaojihusisha na ujangili ikiwa na washiriki 949.

Hata hivyo, Mwaka jana mwanaharakati wa kuhifadhi Wanyamapori raia wa Afrika Kusini, Wayne Lotter, alipigwa risasi na kuuawa maeneo ya nyumbani kwake, Masaki jijini Dar es Salaam na watu wasiojulikana.

Membe, Lowassa wakutana msibani Dar
Wanaoweka rehani watu nchi za nje kitanzini