Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametaja majina ya watuhumiwa wa ujangili ambao wengi wao ni wamiliki na washirika wa Kampuni za uwindaji wa kitalii.

Ameyasema hayo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo ametaja baadhi ya tuhuma hizo ambazo ziko kinyume cha sheria na taratibu za uwindaji wa kitalii kuwa ni uwindaji haramu, udanganyifu kwenye kujaza fomu za uangalizi,  rushwa, uhalifu dhidi ya rasilimali za wanyamapori na uhujumu uchumi.

Ametaja tuhuma zingine kuwa ni ukiukwaji wa kanuni za uwindaji (kupiga wanyama usiku, kuwinda wanyama bila
kujali umri, kupiga wanyama nje ya maeneo waliyopewa), kukutolipa tozo mbalimbali za maendeleo za jamii kwenye vijiji jirani na maeneo wanaoendesha biashara ya uwindaji, kushindwa kuendesha ipasavyo shughuli za kuzuia ujangili.

Aidha, Dk. Kigwangalla amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Pasanis na wenzake ambao wanamilikia kampuni ya Berlette Safari Corporation Ltd na Shein Ralgi na wakurugenzi wenzake wa kampuni ya Game Frontiers of Tanzania Ltd.

Wengine ni Howel na wakurugenzi wenzake wa kampuni ya Mkwawa Hunting Sfaris Tanzania Ltd, Thomas Fredikin na wenzake wa Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd, Wengert Windrose Safaris Tanzania  Ltd na Tanzania Game Trackers Safaris Ltd, na Awadh na wenzake ambao wanamiliki kampuni ya Uwindaji wa Greenmiles Safaris Ltd.

Vile vile amewataja wengine kuwa ni Kwizema, Robert,  Solomon Makulu,  Siasa Shaban, Hamis Abdul Ligagabile na mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Alex Aguma.

Hata hivyo, Dkt. Kigwangalla ametoa Ilani ya siku 30 kwa watu mbalimbali ikiwemo Mawaziri Wakuu
Wastaafu waliovamia kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha wafike kwa Kamishna Mkuu wa Ardhi waweze kuhakikiwa na kuthibitishaumiliki wao halali ama sivyo wavirejeshe Serikalini viweze kumilikishwa kwa mmiliki wake halali.

Mbowe: Mamlaka za sheria zinatakiwa kujitathmini
Magazeti ya Tanzania leo Januari 26, 2018