Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally, amewataka wanachama wa CCM kuheshimu alama za vyama vyote vya siasa nchini kwa sababu vimesajiliwa kisheria.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wakati akizindua mkakati wa kukomaza demokrasia kwenye mashina ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi mkoani humo.

Aidha, amewataka kutochoma wala kubeza alama za vyama hivyo, huku akigusia suala la wafuasi wa vyama vingine kuchoma bendera na kupaka rangi ya chama chao ofisi za chama kingine.

“Chama Cha Mapinduzi tusifanye mambo holela na uhuni huo katika siasa. ni kosa kuparamia na kupaka rangi ofisi za vyama hivyo. CCM tusifanye hivyo ni kosa kisheria,” amesema Dkt. Bashiru.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi wana wajibu wa kulinda uhuru wa vyama vingine vilivyosajiliwa kisheria, hivyo amewaasa kuchana na vitendo ambavyo vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Watu 60 wafariki dunia nchini Ghana
Majaliwa azitaka bodi za mazao kujisajili GS1