Aliyekuwa meneja wa klabu za Rangers na Sunderland Dick Advocaat ametangazwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi la Feyenoord, hadi mwishoni mwa msimu huu.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 72, ametangazwa kushika nafasi hiyo, akirithi mikoba iliyoachwa na beki wa zamani wa Manchester United Jaap Stam, ambaye alichukua maamuzi ya kujiuzulu mwishoni mwa juma lililopita, kufuatia kikosi chake kufungwa mabao manne kwa sifuri dhidi ya Ajax Amsterdam.

Feyenoord wameshinda michezo mitatu kati ya michezo kumi na moja waliyocheza msimu huu, na wanakamata nafasi ya kumi na mbili kwenye msimamo wa ligi ya Uholanzi.

Baada ya kutangazwa kuwa meneja wa klabu hiyo kongwe nchini Uholanzi Advocaat alisema: “Nina uwezo wa kuisaidia klabu hii, nitahakikisha ninafanikisha hilo kwa moyo mkunjufu.”

Naye mkurugenzi wa ufundi wa Feyenoord Sjaak Troost alisema: “Tuna imani kubwa na Dick Advocaat , tutajitahidi kushirikiana naye kwa hali yoyote, ili kufikia mipango na malengo tuliyoikusudia msimu huu, ninafarijika kuona amekubali kuwa nasi hadi mwishoni mwa msimu huu.”

“Tunaamini uzoefu wake wa ukufunzi katika soka, utakisaidia kikosi chetu kurejea kwenye harakati za mapambano na kushinda michezo ilinayotukabili, baada ya kupoteza Jumapili dhidi ya Ajax Amsterdam.”

Abiria wapika chai kwenye Treni, Lalipuka nakuua 70 Pakistan
Video: Afungwa minyororo chumbani miezi miwili,Chadema walalamikia mambo tisa uchaguzi