Kamati ya kombe la Dunia, imemchagua msanii kutoka Tanzania, Diamond Platinumz na wasanii wengine kutoka nchi mbalimbali akiwemo Jason Darulo kutoka Marekani kutengeneza wimbo maalumu wa kombe la dunia (FIFA 2018).

Mashindano hayo ya mpira wa miguu mwaka huu yamepangwa kufanyika nchini Urusi kuanzia juni 14 mpaka julai 15.

Diamond Platinumz akishirikiana na wasanii wengine barani Afrika watafanya wimbo wa Kombe la Dunia uliopewa jina la ”Colours”.

kombe la dunia lililochezwa 2010, Msanii toka Colombia, Shakira ndiye aliyepewa shavu la kutengeneza wimbo huo ambapo alimshirikisha msanii kutoka Afrika Kusini, Freshly Ground ambaye pamoja walifanya kibao cha Waka Waka (This time for Afrika).

Waka Waka ni moja ya wimbo zilizofanya vizuri katika chati za billboard na dunia nzima kwa ujumla na kupata umaarufu na kujulikana zaidi duniani kote kutokana na ubunifu wa hali ya juu uliotumika katika wimbo huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond Platinumz amepost picha ikionesha kombe la dunia akiwa amesindikiza na maneno haya ”2018, #CocaCola”.

Baado hajaliweka wazi swala hili, wala hajazungumzia lolote juu ya ushiriki wake katika wimbo wa Taifa wa Cocacola Fifa 2018.

 

Taifa Stars kuzikabili Algeria, DR Congo
ASFC: Young Africans yapelekwa Singida, Azam FC yabaki D'salaam