Msanii wa muziki bongo fleva na mwanamke mpambanaji maarufu kama Shilole mapema jana amefunga pingu za maisha na Ostadhi maarufu kama Uchebe, ambapo sherehe hiyo imehudhuriwa na  wasanii mbalimbali.

Ambapo baadhi ya wasani waliohudhuria sherehe hiyo ni Diamond Platinumz, Harmonize, Jux, Vanessa Mdee na wengine wengi ambapo kila mmoja kwa nafasi yake alionesha kuithamini siku hiyo kwa kumzawadia zawadi nono.

Diamond Platinum alimpa  nafasi Shilole kuchagua ni zawadi gani angeitaka kutoka kwake, ambapo shilole kama mwanamke mpambanaji alimuomba Diamond amsaidia kuitangaza biashara yake ya pilipili  ya shishi chilly ambayo imeingia sokoni hivi karibuni, na bila shaka Diamond ameahidi kulifanyia hilo kazi.

Aidha Vanessa Mdee yeye ameahidi kuwapeleka wawili hao hyatt regency hotel ‘’honey Moon’’  kwa ajili ya mapumziko mara baada ya kutoka kwenye sherehe hiyo.

Jux naye ameahidi kumlipia ada ya shule ya mwaka mzima mmoja wa mtoto wa Shilole kama namna ya kumpunguzia mwandada huyo majukumu.

Harmonize kutoka kundi la WCB ametoa ahadi ya shilingi milioni tisa ambayo ni thamani ya gari aina ya Noah ambapo amesema itamsaidia kusambaza chakula chake.

Huu ni ushirikiano wa hali ya juu ambapo wasanii wa bongo fleva wanapeana na kuinuana kwa namna moja au nyingine hali ambayo ni tofauti kwa wasanii wa bongo movie ambao bado hawajaanza kula matunda yao wenyewe.

Dkt. Mashinji awajibu wanaosema kiatu hakimtoshi
CCM yajipanga kurudisha Kata zote