Wapenzi wa zamani, Diamond na Wema Sepetu jana waliendelea kuiteka mitandao ya kijamii baada ya kusambaa video ya salamu za kupetipetiana, jana usiku waliibuka na mengine.

Wawili hao ambao walihudhuria ‘Makulusu Challenge’, shindano la kucheza makulusu la mmoja wa wanafamilia wa WCB, Ray Vanny katika ukumbi wa Maisha Basement jijini Dar es Salaam waliwasha cheche nyingine za mapenzi.

Wema alipewa nafasi ya kumkaribisha Diamond Platnumz jukwaani kwa kuwa-surprise mashabiki ambapo aliikamilisha vyema kazi yake na kuzua shangwe kubwa ukumbini hapo.

Hata hivyo, shangwe zaidi iliibuka baada ya Diamond kumpa kumbato la salamu, kukipokea kikuza sauti (microphone) na kisha kuamsha na ‘I love you die’, wimbo alioshirikishwa na Patoranking wa Nigeria.

Uchaguzi huo wa wimbo uliongeza chachu ya shangwe ukumbini hapo kutokana na ujumbe wake wa kumhakikishia mpenzi kuwa unampenda sana hata kifo.

Katika hatua nyingine, Diamond ameandika kwenye Instagram ujumbe wa kutetea alichokifanya yeye na Wema kwenye hafla ya kumkaribisha Mbosso kwenye WCB, akiwataka mashabiki kuelewa kuwa wao ni marafiki na haitaji kudumisha uhasama ndio sababu alimualika Wema.

Hata hivyo, Chibu hakuzungumzia hatua za mapozi ya ndege tetere yaliyoibuka kati yao mbele ya mapaparazi.

Wengi Hupenda kuona watu wakiwa wana Vita ama uhasimu usio na kichwa wala miguu… Eti utamsikia mtu anasema “Dogo Mi shabiki yako Mkubwa na nakukubali sana ila kitendo cha kumualika Wema Umeniuzi” kwaio we unataka mie niendelee kuwa na vita ama niwe na vita na Wema ili iweje? yani mie nikiwa na vita na Wema we unafaidika nini? na itanisaidia ama kusaidia nini kwenye Sanaa yetu? Huwezi kuwa shabiki yangu halaf unafurahia mie kuendelea kuwa na vita na mtu, tena vita ambayo imeshaisha…nina familia yangu Naipenda Naiheshimu na siwezi kuiacha… ila hio sio sababu ya kuwa na vita na watu…na huu ni mfano wa kwanza mwingine unafata…. Huu sio Muda wa kujenga chuki zisizo za msingi ni wakati wa wasanii kushirikiana na kwa pamoja kufanya kazi na kukuza sanaa zetu kwajili ya future ya wadogo na vizazi vyetu vijavyo… Shukran sana Mdam kwakuja usiku wa jana…Mwenyez Mungu akubariki na akujalie kila la kheri uliombalo….. #Watakubali by @Mbosso_ link in his and my BIO

A post shared by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Kenyatta: Ole wake atakayerusha mubashara kuapishwa kwa Odinga
Mbowe: CCM bila Polisi ni wepesi