Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, jana lilimkamata na kumhoji Nasibu ‘Diamond Platnumz’ Abdul kutokana na kusambaa kwa video zake akiwa faragha na wasichana wawili kwa nyakati tofauti.

Taarifa hiyo imetolewa jana bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe amesema kuwa kukamatwa kwa Diamond na kuhojiwa ni matokeo ya kanuni za maudhui ya mitandao ya kijamii zilizosainiwa hivi karibuni na kuwezesha sheria iliyotungwa tangu mwaka 2010 kuanza kufanya kazi.

“Naomba nitoe taarifa kwa wabunge  kwamba kuna baadhi ya wasanii wetu ambao walianza kufanya uhuniuhuni mitandaoni. Jana tumefanikiwa kumkamata msanii nyota, Diamond na amehojiwa kutokana na picha alizoruha. Imebidi Nandy pia ahojiwe na tunaangalia jinsi ya wakuwapeleka mahakamani,” alisema Dkt Mwakyembe.

Nandy aliingia kwenye majanga hayo baada ya video yake akiwa faragha na mwanamuziki mwenzke Billnas aliyekuwa mpenzi wake, kusambaa kwa kasi mitandaoni wiki iliyopita.

Aliwaonya watumiaji wa mitandao hasa vijana kuwa mitandao sio kokolo la kuweka mambo yanayokyuka maadili na utamaduni.

 

Khaligraph Jones aeleza alivyomkwaruza Octopizzo
Video: Diamond Platnumz, Nandy watiwa mbaroni kwa kusambaza video chafu