Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma maarufu kwa jina la Diamond Platnumz ameweka wazi kuwatelekeza watoto wake wawili, Latifah na Nillan kwa sababu mzazi mwenzake, Zarinah Hassan hampi ushirikiano.

Diamond amesema hayo wakati akizungumza katika kituo cha Televisheni cha Wasafi, ambapo amesema kuwa kwa takribani miezi mitatu sasa amesitisha kutoa matunzo ya watoto wake hao wanaoishi nchini Afrika Kusini kwa kuwa mama yao hataki hata aongee na watoto wake wala kuwaleta watoto nchini.

Diamond amesema kila mwezi alikuwa akitoa dola za Marekani 2,000 ambazo ni wastani wa Shilingi za Kitanzania Milioni 5 kwa ajili ya matunzo ya watoto.

“Kiukweli kabisa, nina kama miezi mitatu sijapeleka fedha za matunzo ya watoto kwa sababu mwenzangu hataki hata niongee na watoto, hebu fikiria hata kupitia mfanyakazi wa ndani amegoma nisiongee nao,” amesema.

Amesema anafanya jitihada za kila namna kuhakikisha anawasiliana na watoto wake lakini mwanamke Zari amemuwekea ngumu.

“Nilijaribu kuwasiliana na mtoto wake wa kiume, yule mkubwa (wa Zari) lakini mwenzangu ameniwekea ngumu,” amesema.

Diamond ameendelea kusema kuwa Zari amemuwekea masharti mazito kuhusu kuwaona watoto wake, amesema kuwa akitaka kuwaona watoto wake lazima aje nao nchini (Kwa Diamond) licha ya kwamba Diamond tayari anamahusiano memgine.

“Anataka aje na watoto, nimemwambia Zari nina mahusiano mengine nikamshauri mama yangu mzazi awafuate watoto lakini akakataa akasema labda niende kuwaangalia Afrika Kusini.”

Video: Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu umiliki wa Laini za simu
Serikali kuweka bei elekezi ya Pembejeo za kilimo

Comments

comments