Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Arsenal, Vassiriki Abou Diaby amekataa kufikia makubaliano na uongozi wa West Brom ambao ulionekana kuwa tayari kumsainisha mkataba ili aendelee kubaki nchini Uingereza.

Diaby amekataa kufikia hatua ya kubaki nchini Uingereza, baada ya kudhihirisha amejiunga na klabu ya nchini kwao Ufaransa Olympique de Marseille.

Diaby, ambaye ameitumikia timu ya taifa ya Ufaransa katika mchezo 16, alikua huru baada ya kuachana na Arsenal mwanzoni mwa mwezi uliopita, hali ambayo ilisababisha baadhi ya klabu kuwa na mipango ya kumsajili.

Jana jioni uongozi wa Olympique de Marseille ulithibitisha kufikia makubaliano na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29.

Diaby aliitumikia Arsenal kwa miaka tisa na alicheza michezo zaidi ya 180 na kufunga mabao 19, na msimu uliopita alifanikiwa kucheza michezo miwili.

Platini Kuwania Kiti Cha Urais Wa FIFA
CCM Yajipanga Kuwajibu Chadema Na Lowassa Leo