Klabu ya Tottenham imetangaza kumsainisha mkataba mpya kiungo kutoka nchini England Dele Alli, na sasa atakuwepo White Hart Lane hadi mwaka 2022.

Mkataba mpya kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, utamuwezesha kulipwa mshara wa Pauni 55,000 kwa juma ikiwa ni ongezeko la Pauni 20,000.

Mwezi januari mwaka 2015, Alli alisaini mkataba ambao ulimuwezesha kulipwa kiasi cha Pauni 25,000 kwa juma.

Msimu uliopita Alli alionyesha uwezo mkubwa kisoka na alikua tegemo kubwa kikosini, jambo ambalo lilitoa msukumo kwa meneja Mauricio Pochettino kumuweka kwenye mipango yake ya muda mrefu.

Msimu wa 2015/16, Alli alifunga mabao 10 na kutoa pasi tisa za mwisho zilizozaa mabao yaliyofumngwa na wachezaji wengine wa Spurs.

Mafanikio mengine aliyoyapata kiungo huyo, ni kutajwa kama mchezaji bora mwenye umri mdogo kupitia tuzo za chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England PFA msimu wa 2015/16.

Alli alisajiliwa na Spurs mwaka 2015 akitokea kwenye klabu iliyomkuza ya MK Dons na tayari ameshaitwa kwenye vikosi vya timu za taifa mara 13.

Juma lililopita mshirika wa Alli katika nafasi ya kiungo klabuni hapo Eric Dier alikubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Spurs ambayo imedhamiria kufanya makubwa zaidi ya msimu uliopita ambapo walimaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya nchini England (PL).

Ronaldo, Bale Waongeza Chachu Ya Ushindi Wa 17
SSC Napoli Wamfungia Milango Kalidou Koulibaly