Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, John Polingo ameamuru kuwekwa ndani kwa mkandarasi wa umeme kutoka kampuni ya Cyber, Benjamin John kwa tuhuma za kuchukua fedha kwa wananchi kwa kuwalaghai kuwa atawaunganishia umeme wa REA.

Ametoa amri hiyo kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi baada ya baadhi ya madiwani kudai kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiwatoza wananchi shil. 20,000 hadi 140,000 kwa ajili ya fomu.

Aidha, kutokana na tuhuma hizo, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Erick Ambakisye alilazikmika kuuita uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Songwe kwa ajili ya ufanunuzi.

“Hizi ni tuhuma, naamini vyombo vya dola vitafanya uchunguzi ili ukweli uweze kubainika, ili mambo mengine yaendelee kama ilivyopangwa,”amesema John

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya ameamuru Jeshi la Polisi kumshikilia mkandarasi huyo kwa ajili ya uchunguzi huku akiwataka madiwani hao kuwasilisha ushahidi.

Azam FC yakumbana na adhabu
Waliotaka kumteka Rais waandaliwa nyundo nzito