Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amezindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wajasiliamali wadogo na kuwahakikishia wote wanao stahili kupata vitambulisho kabla ya mwezi kumalizika watakuwa tayari wameshapata.

Akizungumza baada ya kuzindua zoezi hilo lililofanyika mjini Njombe, Msafiri amesema kuwa mara baada ya kusajiliwa na kupata kitambulisho hicho hategemei kuona mjasiliamali yeyote akifanya shughuli zake katika maeneo yasiyokuwa rasmi.

“zoezi hili linaendeshwa kwa maagizo ya mheshimiwa Rais na leo sisi tunazindua sio mwisho lakini hatutalifanya kwa muda mrefu na tunatamani kufikia mwisho wa mwezi huu, wote ambao wanastahili wawe wamechukua vitambulisho hivi na wamekwisha kusajiliwa, na baada ya zoezi hili hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kufanya biashara bila kitambulisho,” amesema Msafiri

Kwa upande wao baadhi ya wajasiliamali wadogo kutoka Halmashauri hiyo akiwemo, Wille Kilasi ambaye ni mlemavu wa miguu wamesema kuwa vitambulisho hivyo vitawasaidia kwa kuwapa unafuu kwa kuwa awali walikuwa wakilipa kodi kubwa kwa mwaka ukilinganisha na mitaji yao.

Okwi, Kagere walivyowapasua JS Saoura 3-0
Video: Matefu amshauri CAG kuitikia wito wa Spika wa Bunge

Comments

comments