Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa kuwaorodhesha wananchi wanaofika kwenye mitaa yao katika daftari maalumu ili kuweza kubaini wahalifu na wahamiaji haramu.

Ameyasema hayo wakati wa kutoa tathmini ya ziara hiyo, ambapo amesema kuwa imebainika maeneo mengine watu wanaishi lakini hawajulikani wanafanya shughuli gani.

Aidha, Mjema alifanya ziara katika Kata 13 za jimbo la Ukonga kuanzia Agosti 13 hadi 18 kusikiliza kero za wananchi na kubaini kuwa baadhi ya maeneo watu wanaonekana usiku tu.

“Kila mwenyekti wa serikali ya mtaa ahakikishe anawajua wakazi wake na kama mgeni amekuja lazima aulizwe atakaa eneo husika kwa muda gani na amekuja kufanya nini. hii itasaidia sana kupunguza uhalifu na wahamiaji haramu ambao wengi huja na silaha,” amesema Mjema.

Hata hivyo, ameongeza kuwa mkakati huo unalenga kupunguza uhalifu katika ngazi ya mitaa kwa vile kumekuwa na matatizo ya wananchi kutishiwa, kukabwa na kuibiwa mali zao.

 

RC Mwanri awaweka kikaangoni Maafisa Ustawi wa Jamii
Serikali yamwaga ajira 2,160 kwa walimu