Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri, ameagiza watoto wote wanaokaa kwenye vibanda vya sinema nyakati za usiku na wakati wa masomo, kukamatwa na kuchukuliwa hatua kali.

Msafiri ametoa kauli hiyo leo Desemba 3, 2019, Jijini Dar es salaam, pamoja na kuwataka wananchi kuwa mstari wa mbele, katika kutoa taarifa zinazohusu matukio ya ukatili wa kijinsia.

Aidha amesisitiza kuwa jamii haina budi kutatua changamoto za migogoro ya kifamilia ili kupunguza idadi ya matukio ya ukatili pamoja na utupaji wa watoto.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, amesema wamebaini uwepo wa matukio 719 ya ubakaji na matukio ya ulawiti zaidi ya 300.

Ufilipino: Hofu yazidi kutanda Kimbunga Kammuri
Kenya: Polisi kizimbani kwa mauaji ya mwandishi wa habari

Comments

comments