Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela leo amefanya ziara Kariakoo jijini Dar es salaam kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kwa jina la Machinga.

Aidha, katika ziara hiyo, Kasesela ameambatana na Mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Juma Abdallah.

Hata hivyo, wametembelea mitaa mbalimbali ya Kariakoo wakiwa na lengo la kujifunza na kupata uzoefu wa namna wilaya hiyo ilivyofanikiwa katika kuboresha mazingira na kuwaweka pamoja Machinga katika shughuli zao.

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Juma Abdallah kwa Machinga wakati wa ziara hiyo
 Baadhi ya kinamama wakimweleza kero Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema alipokuwa na ugeni huo
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika Mtaa wa Kongo kujionea shughuli mbalimbali zinavyoendesha na Machinga wa Kariakoo
 Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela ukipita katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo kujionea shughuli mbalimbali zinavyoendesha na Machinga
 Kasesela akiwa na Mwenyekiti wa Machinga wa kariakoo katika ziara hiyo
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitazama bidhaa za machinga ambazo alisema hadhi ya bidhaa hizo inaonekana ni zaidi na za machinga
 Kasesela akitazama sampuli ya baadhi ya vifaa vya jikoni vinavyofanya kazi ambavyo anauza Machinga
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ricard Kasesela akihoji mfumo kwenye kompyuta alipoingia katika Ofisi ya Umoja wa Machinga kujua wanavyofanya kazi.
Machinga ambaye ni mtaalamu wa programu za kompyuta Namoyo Yusuf, akimpa maelezo Kasesela ya namna ambavyo Umoja wa Machinga unavyohifadhi kumbukumbu zote za machinga katika komyupta. Kulia ni Mbunge wa Kilolo Asia Juma akifuatilia kwa karibu
 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Juma akimweleza jambo Ofisa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya walipokuwa kwenye Ofisi hiyo ya Machinga Kariakoo
 Kasesela na ujumbe wake wakitoka katika Ofisi ya Machinga
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela na Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Asia Juma wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Machinga wakati wa ziara hiyo
 Kasesela akimfurahia Ustadhi ambaye ni mmoja wa machinga Kariakoo
 Kasesela akifurahia jezi la Timu ya Machinga baada ya kuzawadiwa katika ziara hiyo
 Kasesela na Amina wakichagua nguo kwenye vitalu vya biashara za Machinga wakati wa ziara hiyo
 Kasesela akilipa fedha baada ya kuchagua nguo alizopenda
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiagana na Mwenyekiti wa Machinga Stephen Lusinde mwishoni mwa ziara hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akifanya majumuisho na ujumbe wake bada ya kurudi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akifanya utambulisho na kutoa maelezo machache kabla ya kuanza ziara hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza ofisini kwake na ujumbe huo kabla ya ziara hiyo kuanza
 Kasesela akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kabla ya ziara kuanza
Kasesela na ujumbe wake wakijiandaa kuondoka ofisi kwa Mkuu wa wilaya kuanza ziara hiyo.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 23, 2018
Makonda akemea kunyosheana vidole shambulio la Akwilina, aagiza kupisha uchunguzi