Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga, amemchapa viboko mzazi wa mmoja wa watoto walioshambulia kwa mawe gari yake na kuvunja kioo.

Kufuatia kupasuliwa kwa kioo hicho, mkuu huyo wa wilaya alisimamisha gari na kuwakimbiza watoto hao hali iliyozua taharuki kubwa kwa wananchi.

Aidha, mmoja wa wazazi wa watoto walishambuia gari hilo alipohojiwa na DC huyo, alionyesha jeuri ndipo alipoamua kumcharaza viboko.

“Malezi, malezi gani unataka kwangu? mtoto ametoka shule nitajuaje anayoyafanya mtaani,”alijibu mzazi huyo

Hata  hivyo, akizungumzia tukio hilo, Odunga amesema kuwa kwa sasa wanajipanga kwaajili kkufanya opresheni ya kuhakikisha tabia hiyo inakomeshwa.

Majaliwa akemea matukio ya uhalifu Ulyankulu
LIVE: Yanayojiri uchaguzi mkuu wa TFF Dodoma

Comments

comments