Mkuwa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, Adrea Tsere ameeleza kushangazwa na uongo aliouita uzushi na kusema kuwa unaenezwa na wabaya wake ambao wameamua kufanya hivyo ili kumrudishaa nyuma katika jitihada zake za kupambana na wala rushwa katika wilaya hiyo.

Tsere amesema hayo kufuatia taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa alijikuta amelala chooni katika mazingira ya kutatanisha.

Taarifa hizo zilizosambaa zimeeleza kuwa Tsere amefanyiwa kitendo hicho kutokana na tambo na  mbwembwe zake za hali ya juu ambapo tambo hizo zilikuwa zikiwakera wazee, tambo hizo ni pamoja na kauli zake za mara kwa mara kuwa ameaga kwao hivyo wasijaribu kumchezea kwa njia za ushirikina kwani yuko vizuri, pia anadaiwa kuwakera watu wa wilaya hiyo kwa kauli yake kuwa vijana wengi wameathirika na Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa ujinga wao na amekuwa akikamata wananchi hovyo na kuwaweka ndani.

Wazee katika wilaya hiyo wamekuwa wakimuonya lakini akawa jeuri ndipo wakaanza kumfanyia vituko kwani alipoamka asubuhi alijikuta chooni kalala hapo na mdomo upo kwenye tundu la choo tena cha nyumba ya wageni (Guest House), Na baada ya siku kadhaa akafuata mkewe kisha watoto na utaratibu ukaendelea hivyo hivyo.

Hata hivyo, Tsere amekanusha taarifa hizo na amesema hatishwi na uzushi huo, ataendelea kupambana na wote wanaovunja sheria katika wilaya hiyo wala hawezi kuomba uhamisho kwa uzushi huo kama ambavyo waliozusha wanatarajia.

Aidha amesema kuwa ataendelea kusimamia haki na kuzingatia weledi bila kumuonea mtu na hata kama hao wazushi wataibua uzushi hautafanikiwa kwani anaamini Mungu na hamtendei mtu ubaya wala kumuonea mtu.

 

Video: Waziri ataja mikoa 10 kuhusu Saratani
#HapoKale

Comments

comments