Mwanamuziki kutoka Nigeria Davido ametoa burudani katika jukwaaa la Hot 97 katika tamasha la Sammer Jam lilofanyika Marekani ambapo Davido alipata nafasi ya kupanda jukwaa moja na wakali kama Cari B , Meek Mill, Migos, Tory Lanez, Rich The Kid na wakali wengine kibao.

Inaelezwa kuwa ili kupata tiketi ya kuwaona wakali hao juu ya stage ilipaswa mtu wa kawaida kulipia kiasi cha thamani ya dola za Kimarekani 234 ambayo ni  sawa na zaidi ya shilingi laki tano za Kitanzania.

Aidha wimbo wa Fall wa Davido ulitajwa kuwa ndio wimbo wa kwanza kutoka kwa msanii huyo kuwahi kukaa muda mrefu zaidi kwenye chart za Billbord ukilinganisha na nyimbo nyingine za Afrobeats ambazo ziliwahi kukaa kwenye chart hizo.

Hata hivyo January 28, 2019 iliripotiwa kuwa Davido alishika nafasi ya pili kuujaza uwanja wa O2 mjini London Uingereza baada ya Wizkid kuujaza uwanja huo huku akivunja rekodi ya kuwa msanii wa kwanza mwenye umri mdogo katika bara la Afrika kuujaza uwanja huo.

Cardi B kukumbwa na kashfa iliyomponza R Kelly
Davido, J Cole kupanda jukwaa moja katika tamasha la DreamvilleFestival
Davido jukwaa moja na Cardi B, Future
Jay Z awa rapa wa kwanza kuwa bilionea
Askofu Gwajima akutana na JPM Ikulu, afunguka 'lazima uvunje mayai'

Comments

comments