Wakala wa Mabasi ya mwendokasi (DART), wamewataka abiria wote wanaotumia mabasi hayo, kutoka maeneo ya Kimara kuelekea mjini wabadilishe njia kwa kutumia mabasi hayo hadi Morocco na wakishafika hapo, wachukue usafiri mwingine utakaowafikisha mjini.

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 16, 2020, kufuatia uwepo wa mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo, na kupelekea eneo la Jangwani kujaa maji na hivyo barabara hiyo kutopitika.

Haya ni baadhi ya maeneo yaliyoathirika na mvua za leo

“Tunawashauri wasafiri wa mabasi ya Mwendokasi wanaotokea Kimara kuelekea mjini-kati kuwa watumie mabasi hayo mpaka Morocco, halafu wachukue usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka mjini-kati, Kariakoo na sehemu nyingine za jiji.”

Hivyo hivyo, wale wanaotokea mjini-kati kwenda Kimara, wachukue usafiri mbadala mpaka Morocco ambapo wanaweza kuendelea na usafiri wa mabasi ya Mwendokasi kuelekea Kimara” imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imeeleza kuwa mvua iliyonyesha leo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara, itaendelea kunyesha hadi Januari 17, 2020.

Lukuvi atumbua jipu: Benki zinavyotumia madalali kutapeli nyumba Dar
Haya ni baadhi ya maeneo yaliyoathirika na mvua za leo