Beki wa kulia kutoka nchini Brazil Dani Alves, atazikosa fainali za kombe la dunia zitakazoanza rasmi Juni 14 nchini Urusi, kufuatia majeraha ya goti alioyapata akiwa katika majukumu ya kuitumikia klabu yake ya PSG.

Alves alilazimika kutolewa uwanjani kwa machela, wakati wa mchezo wa fainali ya kombe la Ufaransa (Coupe de France), uliowakutanisha dhidi ya  was Les Herbiers waliokubali kisago cha mabao mawili kwa sifuri siku ya jumanne.

Siku ya jumatano msemaji wa klabu ya PSG alithibitisha uhakika wa beki huyo kuziwahi fainali za kombe la dunia, kutokana na vipimo alivyofanyiwa, lakini jana Ijumaa ilithibika rasmi Alves hatoweza kucheza fainali hizo, na atafanyiwa upasuaji.

Kwa mantiki hiyo Alves hatofanikisha lengo la kucheza fainali za mwaka huu, ambazo alikua amezidhamiria kama sehemu ya historia yake ya kucheza michuano hiyo ya dunia kwa kutangaza kustaafu.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Tite atalazmika kufanya uteuzi wa mchezaji mwingine anaecheza nafasi ya beki wa kulia, ili kuziba pengo linaloachwa wazi na Dani Alves.

Bwawa lililobomoka na kuua makumi Kenya lilijengwa 'kihuni'
Video: Mikopo elimu ya juu wabunge wachachamaa, Makinikia yaleta kiama

Comments

comments