Benki ya CRDB imeanzisha bidhaa tatu mpya kwa wateja wake ikiwamo  wenye vikundi vya vikoba kupata akaunti kupitia simu zao za mkononi ili kuondokana na changamoto zinazowakabili.

Meneja wa Huduma za Fedha kwa Njia ya Mtandao wa CRDB, Edith Metta, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari kuhusu  huduma hizo mpya.

Alizitaja huduma hizo kuwa ni akaunti ya kikundi, akaunti ya akiba na akaunti ya malipo.

Metta alisema kumekuwa na changamoto katika baadhi ya vikundi vya fedha ikiwamo vikoba za kupotea kwa fedha au mmoja kukimbia nazo, hivyo wameamua kutoa  suluhisho kwa vikundi ili fedha zao ziwe salama.

Alisema wanachama wana uwezo wa kufungua akaunti ya pamoja kupitia simu zao za mkononi na kisha kusajili jina la kikundi na kuanza kuweka fedha pamoja na kutoa bila makato.

“Mwanachama wa kikundi ana uwezo wa kuangalia salio katika akaunti ya kikundi na endapo kuna fedha imetolewa kinyemela wanajua kwa wakati na kuepusha mwanachama kukimbia na fedha au kuambiwa fedha zimeibwa,” alisema.

Alisema akuanti ya kikundi ni nzuri kwa kuwa fedha zinakuwa salama na endapo kunakuwa na udanganyifu wanajua mapema na kuanza kuchukua hatua.

Kagame awaachia huru mkosoaji wake na aliyepanga kumuua
LIVE: Uzinduzi Tamasha la Urithi Festival