Imeelezwa kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya virusi vya corona nchini Italia inaongezeka kila uchao.

Hadi kufikia jana Jumamosi watu 800 walikufa, na kuifanya idadi jumla kufika karibu watu 5,000 ambao wamefariki kutokana na homa ya COVID 19 nchini humo.

Kufuatia hali hiyo, serikali ya nchi hiyo imeamrisha biashara zote kufungwa hadi ifikapo Aprili 3.

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte amesema kupitia video iliyoruishwa kwenye mtandao wa Facebook kwamba wakati huu ni mbaya kuwahi kutokea tangu baada ya kumalizika vita vya dunia, na kuongeza kwamba shughuli za kibiashara zilizo muhimu ndizo zitaruhusiwa kuendelea kufanya kazi.

Tangu Alhamisi iliyopita, Italia ilichukua nafasi ya kwanza na kuipita China kwa idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya virusi hivyo vya corona.

Video: Mapadri 30 wafariki kwa Corona, Dkt. Slaa atoboa siri alivyojiuzulu Chadema
Corona: Zanzibar yazuia safari za watalii

Comments

comments