Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amesema mlipuko wa virusi vya Covid- 19 ni tishio kwa sekta ya Utalii nchini.

Amewataka Watalii wa mataifa mbalimbali waliokuwa wamepanga kuja nchini kutositisha safari za kuja nchini bali wasogeze mbele.

Tanzania hadi sasa imeripoti Wagonjwa 6 waliopata maambukizi ya virusi hivyo ambapo miongoni mwao, mgonjwa mmoja yupo Arusha na wawili wapo Jijini Dar na Zanzibar.

Jana Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo amesema licha ya Zanzibar kutegemea sekta ya Utalii katika uchumi wake wamelazimika kuzuia safari zote za watalii.

Hadi hivi sasa mataifa 52 kati ya 54 barani Afrika tayari yamesharekodi kupatikana kwa virusi vya corona, na  Watu zaidi ya 1000 wameambukizwa kote barani Afrika.

Dkt. Tulia atembelea waliokumbwa na mafuriko Mbeya
Video: Mapadri 30 wafariki kwa Corona, Dkt. Slaa atoboa siri alivyojiuzulu Chadema

Comments

comments