Visa vipya 21 vya wagonjwa wa covid 19 nchini Uganda vimeongezeka na kufanya idadi ya wagonjwa kuwa 160 baada ya kupima sampuli 1,896 jana, Mei 14, 2020.

Kati ya sampuli hizo, 1,593 zilitoka kwa madereva wa malori na 303 ni sampuli kutoka katika jamii za watu wa Uganda.

Wagonjwa wapya wote ni madereva wa malori, na kati ya wagonjwa hao wapya 8 ni Wakenya, 7 ni Watanzania, 5 ni Waganda na mmoja anatokea Sudan Kusini.

Imeelezwa kuwa waliingia Uganda kupitia mipaka ya Mutukula, Busia na Elegu.

Aidha, Wizara ya Afya nchini humo imetangaza kuwa wagonjwa 63 wamepona tangu mgonjwa wa kwanza wa covid 19 alipobainika huku kukiwa hakuna kifo.

Chadema watangaza hatua ya kwanza baada ya kutoka karantini
Msumbiji: Jeshi la Serikali lawaua wanamgambo 50