Shirikisho la Soka nchini Hispania (RFEF) limetangaza kutoa Euro milioni 500 (zaidi ya shilingi trilion 1.2 za Kitanzania) kwa ajili ya kuzisaidia klabu zilivyo kwenye hali ngumu ya kifedha, kusadia mapambano dhidi ya janga la #Corona.

Fedha hizo zitatolewa kwa klabu ambazo zitashindwa kupata faida inayotokana na haki ya matangazo ya televisheni katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama, na vitatakiwa kurejesha fedha hizo ndani ya miaka mitano ijayo.

Shirikisho hilo pia limesema litatoa paundi milioni 3.7 (zaidi ya shilingi bilioni 10) kwa timu zisizoshiriki ligi za kulipwa (non-professional men’s and women’s teams).

“Tutakaa na #Laliga kujadili tatizo hili la kifedha linaloweza kuzikumba baadhi ya klabu… Ujumbe wangu ni umoja, matumaini, nidhamu. Wadau wote wa soka katika ngazi zote, tunapaswa kusambaza ujumbe wa ushirikiano, kwa pamoja tutakidhibiti kirusi hiki”, kauli ya Rais wa RFEF, Luis Rubiales.

Rais huyo pia ameruhusu hoteli ya timu ya taifa ya Hispania pamoja na watumishi wake wote wakiwemo wataalamu wa saikolojia na viungo, kutumiwa na serikali katika huduma za afya kukabiliana na ugonjwa wa Covid_19.

Hadi kufikia jana Jumatano, idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi vya Corona nchini Hispania imefikia  3,434, ikiipiku China kwa vifo 738 na hivyo kuwa taifa la pili kwa vifo vingi nyuma ya Italia.

Kenya: Serikali yapiga marufuku uuzaji wa Chloroquine
Mbowe ajiweka karantini na familia yake