Mwanamuziki mgongwe wa DRC, Aurlus Mabele maarufu kama Mfalme wa Sokous amefariki dunia saa chache zilizopita jijini Paris nchini Ufaransa, huku kukiwa na taarifa kuwa huenda kifo chake kimesababishwa na virusi vya corona (Covid-19).

Mwanamuziki huyo ambaye taarifa zilizothibitishwa na familia yake zimeeleza kuwa alikuwa anasumbuliwa na tatizo la saratani ya koo kwa muda mrefu, alifariki jana, Machi 19, 2020 akiwa na umri wa miaka 67.

Mabele ndiye mwanzilishi wa kundi la Loketo lililoanza kutamba tangu miaka ya 1980, kundi ambalo lilifanya vizuri huku nyimbo zao zikivuka mipaka ya Afrika kwa kasi.

Mwandishi maarufu aliyekuwa nchini Ufaransa, Robert Brazza alithibitisha kifo cha mwanamuziki huyo na kutoa salamu zake za rambirambi.

“Hello mjomba Aurlus, hakika sitasahau ushauri wako, ulisema ‘kuwa salama mdogo wangu na furahia’. Majonzi yangu ni makubwa usiku huu lakini heshima yangu kwako ni kubwa zaidi. Ulikuwa furaha, ulikuwa w

ema. Daima. Nenda kwa amani Aurlus Mabelle. Ninafahamu shangazi Nzambi ameshakukaribisha tayari kwenye rehema,” aliandika kwenye Facebook.

Taarifa kuwa huenda amefariki kutokana na virusi vya corona zimekuja wakati ambapo Ufaransa imeshuhudia vifo vya watu 371 kutokana na virusi hivyo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Wakala wa Afya nchini humo, visa vya corona vimeongezeka hadi 10,995 kutoka 9,134, ikiwa ni ongezeko la 20% ndani ya saa 24.

Video: Wagonjwa wa Corona waongezeka Tanzania, Membe akoleza moto wa tume huru
Membe aibuka tena na uchaguzi 2020, aeleza alichosema alipohojiwa