Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel (65) amejiweka Karantini nyumbani kwake baada ya kukutana na Daktari ambaye amethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Daktari huyo alienda kumpa Merkel chanjo ya Homa ya Mapafu (Pneumonia) siku ya Ijumaa na baada ya Markel kujua Daktari huyo amepata maambukizi Kansela ameamua kujitenga mwenyewe.

Awali, Nchi ya Ujerumani kupitia kwa Kansela huyo ilizuia mikusanyiko ya watu zaidi ya wawili ikiwa ni hatua ya kupambana na Covod 19.

Kansela alisema, zuio hilo ni sahihi zaidi kuliko kuwataka watu wabaki nyumbani. Watakao kiuka wanaweza kupata adhabu.

Mkusanyiko wa watu zaidi ya wawili unaoweza kuruhusiwa ni wa watu wa familia moja wanaoishi pamoja. Pia, watu wametakiwa kuongea wakiwa umbali wa mita 1.5 hadi 2.0

Zaidi Merkel amesema migahawa, saluni na maduka ya wachora tatuu yatafungwa.

Kifo cha Dkt. Makongoro Mahanga, Chadema watoa taarifa
Video: watakaoingia nchini sasa kutengwa, Askofu Katoliki amuwashia moto Polepole

Comments

comments