Wakati mchezo mkali kati ya Chelsea na Arsenal ukitarajiwa kupigwa siku ya Jumapili kocha wa klabu ya Chelsea Antonio Conte amesema anaipa kipaumbele Arsenal, kuwa moja kati ya klabu zitakazoleta upinzani mkubwa katika kuwania taji la ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

Wakati Antonio Conte akiiwezesha Chelsea kutwaa ubingwa wa ligi kuu katika msimu wa kwanza tu akiwa na timu hiyo Aresene Wenger klabu yake ilimaliza msimu uliopita ikiwa pointi 18 nyuma ya mabigwa hao.

Arsenal walifanikiwa kumaliza msimu wakiwa mabigwa wa kombe la FA kwa kuwafunga Chelsea katika mchezo wa fainali lakini klabu hiyo ilimaliza msimu ikiwa nafasi ya tano na kushindwa kupata nafasi yakushiriki katika michuano ya klabu bingwa.

Hata hivyo Antonio Conte anaamini pamoja na Arsenal kuanza ligi vibaya ikiwa imeruhusu kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Liverpool bado klabu hiyo inaweza kupigania ubingwa wa Uingereza.

”Sioni ni kwanini wasiwe mabigwa, wamempoteza mchezaji mmoja tu Oxlade-Chamberlain na bado wamebaki na wachezaji wazuri wa kiwango cha juu wanaweza kupigania ubingwa”, alisema Conte.

Chelsea na Arsenal zitakutana Jumapili ya wiki hii tarehe 17 katika mchezo wa kigi kuu ‘EPL’ na mara zote Arsenal imekuwa ikitoa upinzani mkali kwa Chelsea tangu klabu hiyo iwe chini ya Conte.

 

 

Rash Don aanika ukweli Studio ya Suprise Music
Tanzania yakanusha vikali kuwa na uhusiano na Korea Kaskazini

Comments

comments