Kituo cha CNN kimeshuka chini na kuomba msamaha kufutia kauli yao ya kuitaja Kenya kama ‘kitovu cha ugaidi’ wakati wa maandalizi ya rais Barack Obama kuitembelea nchi hiyo.

Rais Uhuru Kenyata, wiki hii aliwafurahisha wakenya waliokasirishwa na kauli ya CNN ambao walitumia mtandao wa twitter kuonesha hasira zao kwa kutumia hashtag (#SomeoneTellCNN).

Rais Kenyatta alitumia mtandao huo kuwaeleza CNN kinagaubaga kuwa waliiudhi serikali ya Kenya na wakenya kwa ujumla huku akiipoza hasira yake kwa kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho cha runninga cha Marekani kuitembelea Kenya na kuweka ofisi yake kwa kuwa ni mahali salama.

national

Vikumbo vya rais Kenyatta zimezaa matunda ambapo Mkurugenzi Mtendaji CCN amejitokeza na kuomba msamaha kwa kile kilichofanyika. National Fm ya Kenya imeandika katika ukurasa wake wa Twitter kile kilichotokea.

De Gea Apasua Ukweli Wa Kuwekwa Benchi
Hatimaye Octopizzo Awashinda Dr. Dre Na Beyonce, Avunja Rekodi iTunes