Mkurugenzi  wa Clouds Media  Group Joseph Kusaga  amezungumzia lengo kuu la kuleta shindao kubwa la kutafuta vipaji  Afrika Mashariki litalojulikana kama East Africa got Talent na kuhusisha vipaji vya aina zote.

Amesema kuwa mara zote kumekuwa na mashindano ambayo ni ya kuimba tu bila kuangalia kuwa kuna vipaji vingine tofauti na kuimba lakini ameongeza kuwa  clouds ndio iliyokuja na ‘agency’ ya kwanza ya masuala ya mitindo hiyo miaka 22 iliyopita.

Ameongea kuwa Clouds iliwasiliana na serikali  juu ya kufanya fainali hizi apa nyumbani  lakini kulikuwa na sababu za msingi kuipeleka Kenya moja ikiwa ni miundombinu inayoruhusu uzalishaji wa tukio hilo ambapo fainali za EAGT zitafanyika nchini Kenya huku washiriki wakitoka katika nchi nne Tanzania, Kenya Uganda na Rwanda

Waziri wa habari sanaa na michezo Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa  East Africa Got Talent (EAGT) ni tukio muhimu sana katika kuitangaza nchi yetu na vivutio vyake.

Aidha amewapongeza  Clouds media kwa mara nyingine tena wametutoa kimasomaso katika kuitangaza Tanzania na kuibua vipaji kwa vijana.

Record lebal ya kwanza ya muziki ilitokea ndani ya Clouds na baadae kituo cha kwanza cha burudani tulianzisha sisi  kwahiyo tumeona huu ni wakati muafaka kwa sisi kuwa wakwanza kuleta shindano  kubwa Zaidi duniani, amesema  kusaga

Kampuni  ya Rapidblue  ndio wanazalishaji  vipindi vya  South Africa Got Talent na matukio mengine  makubwa  ambapo watashirikiana na Clouds media katika uzalisha wa matukio yote ya  East Africa Got Talent

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 11, 2019
Magufuli atengua na kusamehe Njombe