Muimbaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Christian Bella amezungumzia jinsi alivyo anza kuzikimbiza ndoto zake za kuwa mwanamuziki mkubwa barani Afrika, mbio zilizotua kwenye mazoezi ya bendi ya Mkongwe wa muziki wa dansi, Koffi Olomide.

Bella ambaye kwasasa ni moja kati ya wasanii wenye mafanikio nchini Tanzania amesema wakati anaanza muziki alipata fursa ya kufanya mazoezi na bendi ya Koffi lakini hakuweza kupata nafasi ya kujiunga na bendi hiyo.

Akizungumza na kipindi cha Nipe 5 kinacho ruka kupitia TBC FM, Bella amesema ilikuwa ngumu kupata nafasi kwenye bendi ya mkongwe huyo kwa kibindi hicho kutokana na kuwepo kwa wasanii wengi wenye uwezo zaidi.

“Ilikuwa ngumu mimi kujiunga na bendi ya koffi kwasababu kulikuwa na watu wengi wanaweza kama Fally Gola na wengine wengi, lakini walikuwa wakinipa nafasi nafanya kweli,’’amesema bella ambaye  aliachia wimbo aliomshirikisha Koffi olomide, ‘Acha Kabisa’.

Kwa mujibu wa Bella, kwa sasa Koffi anatamani ajiunge na bendi yake lakini kwa sasa hawezi kufanya hivyo kwani ameshakuwa na kazi nyingi binafsi anazotaka kuzimamia kama mwimbaji binafsi.

Bella ni Bosi wa Malaika Bendi ambayo imewaajiri waimbaji wengi wa ndani na nje ya nchi lakini jina lake linaendelea kuonekana kuwa kubwa zaidi ya bendi yake.

Wakuu wa Wilaya waagizwa kusimamia wakulima Tumbaku
Trump aalikwa pambano la Mayweather Vs McGregor

Comments

comments