Mwanamuziki mkubwa na maarufu Marekani na duniani kote, Chriss Brown ameomba msanii wa muziki Uganda Edris Musuuza maarufu kama Eddy Kenzo Kushiriki katika video ya wimbo mpya anaotarajia kuachia hivi karibuni.

Chriss Brown amemuomba amshirikishe katika video ya wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la ”Back in love”.

Hivyo amefikisha maombi hayo kupitia menijimenti yake kwa kushirikiana na Nick Jackson ambaye ni meneja wa kampuni ya utayarishaji wa muziki inayofanya kazi na Chriss Brown.

Mara baada ya kupokea barua hiyo, Kenzo alikuwa na furaha kubwa na kurusha katika mitandao ya kijamii  barua hiyo iliyomtaka kufanya video na Chris brown.

”Industri yetu sasa inajulikana kila sehemu sababu ya style ya Kenzo,  wasanii wote wanataka kufanya kazi na sisi…tufanye kazi kwa bidii tukiamni tutafanikiwa” aliandika Eddy Kenzo kupitia ukurasa wake wa facebook.

Aidha kwa mujibu wa maelezo kwenye barua hiyo, Chriss Brown amemfahamu Eddy Kenzo kupitia mtandao wa You Tube mara baada ya kuangalia video yake katika wimbo wa Sitya Loss, na kumtaka kufanya naye kazi katika ujio wa nyimbo yake ya Back in love.

Mbali na Kenzo Chriss Brown pia ameomba kikundi cha watoto nchini Nigeria kinachojihusisha na mausala ya Dance ”Ghetto Kid” kushiriki katika video hiyo.

Both Eddy Kenzo na Ghetto Kids wamepasua anga kimataifa baada ya video ya wimbo wa ‘Sitya loss’.

Wimbo huo umefungua milango kwa Eddy Kenzo na kumfanya ashinde katika tuzo za BET mwaka 2015, kwa msanii bora chipukizi.

 

Wachimbaji wa dhahabu Namungo wapewa somo, 'Tunzeni mazingira'
BBC yafungiwa kufanya kazi Burundi

Comments

comments