Albam mpya ya Chris Brown ‘Heartbreak on a Full Moon’ imeweka rekodi ya kupewa kiwango cha mauzo cha ‘gold’ na kampuni ya Industry Association of America (RIAA).

Albam hiyo ambayo ndani yake wanasikika Future, R. Kelly na Jhené Aiko imeuza zaidi ya nakala 500,000 hadi kufikia Novemba 8 mwaka huu, kwa mujibu wa RIAA.

Heartbreak on a Full Moon’ pia imeshika nafasi ya tatu kwenye Billboard 200 ndani ya wiki tatu tangu iachiwe rasmi.

Nyimbo tatu kutoka kwenye albam hiyo hadi sasa ziko kwenye chati ya Billboard Hot 100, ikiwa ni pamoja na ‘Pills and Automobiles’ aliyowashirikisha Kodak Black, Yo Gotti na A Boogie Wit Da Hoodie’ imeshika nafasi ya 51.

‘Questions’ imeshika nafasi ya 79 na ‘High End’ aliyowapa shavu Future na Young Thug imefunga namba 100.

Baba yake Kanumba: Nimeota Lulu ataachiwa huru
Usajili timu za wanawake watangazwa