Mshambuliji Obrey Chirwa amevunja ukimya kwa mashabiki wanaomponda kuwa amegoma kushinikiza kupewa mkataba mpya mnono zaidi.

Chirwa ndiye kinara wa ufungaji wa Yanga kwa sasa kwenye ligi akifunga mabao 11 na amekuwa mchezaji muhimu kwa mabingwa hao hasa baada ya nyota kadhaa kuwa majeruhi.

Mzambia huyo hakujumuishwa kwenye kikosi cha Yanga kilichokwenda Shelisheli kwa ajili ya mchezo wa maruadiano dhidi ya St Louis keshokutwa Jumatano kutokana na kuwa majeruhi.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo umemnukuu nyota huyo akilalamikia mashabiki ambao wanadhani kuwa amegoma.

“Sijawahi kusema wala kumwambia mtu kuwa nataka milioni 150 kwa ajili ya mkataba mpya, sipendezwi na namna wanavyonizushia nadhani nia yao ni kunigombanisha na wapenzi wa Yanga.

“Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Majimaji ajabu wanasema nimegoma, huu ni upuunzi. Mimi ni mchezaji wa Yanga, mimi na klabu ndio wenye kujua hatima yangu ya baadae, niacheni nicheze mpira,” alinukuliwa Chirwa.

Familia yaridhia kuuzika mwili wa Akwilina
Infantino kuongoza mkutano wa FIFA akiwa Tanzania