Rais wa China Xijinping amemtaka rais wa Marekani, Donald Trump kuchunga matamshi yake na vitendo vinavyozidisha hali ya kuzua wasiwasi katika mgogoro unaoendelea baina yake na Korea Kaskazini.

Rais Trump na Korea Kaskazini wamekuwa katika mgogoro wa kurushiana maneno kwa muda mrefu, ambapo rais huyo wa Marekani amekuwa akitishia kuishambulia Korea Kaskazini.

Kwa upande wake, China ambayo ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini imemtaka Rais Trump kupunguza ukali wa maneno ambayo yanaweza kusababisha madhara makubwa katika mgogoro huo.

Marekani na China zilikubaliana kwamba Korea Kaskazini inatakiwa kusitisha mpango wake wa majaribio ya silaha za nyuklia na masafa marefu ambazo zimekuwa ni tishio kwa usalama.

Hata hivyo, Hofu kubwa imetanda kuhusu mpango wa kinyuklia mara baada ya Korea Kaskazini kuzidisha majaribio baada ya makombora yake ya masafa marefu mnamo mwezi Julai.

Live Breaking News: Wallace Karia aukwaa urais wa TFF
Serikali yapiga marufuku ugawaji maeneo

Comments

comments