Chin Bees leo anazindua album yake mpya ‘Ladha’ ndani ya Club Next Door iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Rapa huyo ambaye pia anafahamika kwa uwezo wake mkubwa wa uandishi wa nyimbo, yupo chini ya kampuni ya Wanene Entertainment ambayo inatajwa kuwa moja kati ya makampuni bora zaidi na makubwa ya muziki Afrika Mashariki.

Bees ameiambia Dar24 kuwa kwenye uzinduzi huo ambao utahudhuriwa na mastaa kibao atagawa bure nakala za albam hiyo kwa mashabiki wakataohudhuria pamoja na kuionesha kwa mara ya kwanza video ya wimbo wake mpya.

Ney wa Mitego: Najiona nikienda kuacha kazi ya muziki.

Madaktari bingwa waleta mgomo

Katika kipindi cha miaka miwili, Chin Bees anayetokea Arusha, ameibuka kuwa mmoja wa waimbaji waliochupikia kwa kasi huku nyimbo zake Pepeta, Kababaye, Nyonga na zingine zikimweka juu.

‘Ladha’ itakuwa na jumla ya nyimbo 11 ambazo ni pamoja na Leo, Killer, Nitulize, My Baby, Check It, Cynthia, Ladha, Msafiri, Sqwizza, Zungusha na Mororo.

 

 

Madaktari Kenya wasimamishwa kazi kwa uzembe
Ney wa Mitego: Najiona nikienda kuacha kazi ya muziki.