Baada ya kichapo cha mabao matatu kwa sifuri kilichotolewa na Man city, klabu ya Chelsea ilikamilisha usajili wa beki kutoka nchini Ghana na klabu ya Augsburg ya nchini Ujerumani, Abdul Rahman Baba.

Chelsea, walikamilisha dili hilo kwa paund million 21.7, baada ya kuafikiana na viongozi wa Augsburg mwishoni mwa juma lililopita, kufanya biashara ya kuuzwa kwa beki huyo ambaye ni sehemu ya wachezaji vijana wanaoitumikia timu ya taifa ya Ghana chini ya umri wa miaka 21.

Dakika chache baada ya mchezo wa ligi ya nchini England kumalizika kwenye uwanja wa Etihad, Chelsea walithibitisha kumsajili beki huyo ambaye jina lake lilikua likitawala katika baadhi ya vyombo vya habari kwa kuhusisha na mpango wa usajili huko Stamfod Bridge.

Rahman, anaondoka nchini Ujerumani baada ya kusajiliwa na Augsburg miezi 12 iliyopita, ambapo alishuhudiwa akitokea kwenye klabu ya Greuther Fürth inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo.

Rahman ni matunda ya kituo cha kulea na kuendeleza vipaji kwa vijana cha Asante Kotoko ambacho kipo nchini Ghana.

Diamond Azungumzia Barua Inayodai Tiffah Sio Mwanae
Yanga Kuiwahi Azam FC Dar es salaam